Linus Siwiti's podcast: Recent Episodes

Linus Siwiti

This podcast special for spiritual, social motivation, physical, lesson

View Details

1 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.
Ufunuo wa Yohana 2:1

2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;
Ufunuo wa Yohana 2:2

3 tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka.
Ufunuo wa Yohana 2:3

4 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.
Ufunuo wa Yohana 2:4

5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
Ufunuo wa Yohana 2:5

6 Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia.
Ufunuo wa Yohana 2:6

7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
Ufunuo wa Yohana 2:7

8 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai.
Ufunuo wa Yohana 2:8

9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
Ufunuo wa Yohana 2:9

10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
Ufunuo wa Yohana 2:10

11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Ufunuo wa Yohana 2:11

12 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
Ufunuo wa Yohana 2:12

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
Ufunuo wa Yohana 2:13

View Details

Mambo matatu ya kufanya unapopitia changamoto katika Biashara au Ujasiriamali:
1. Badilisha mfumo wa biashara,
2. Boresha Biashara yako
3. Tumia changamoto kuzigundua fursa zingine.

View Details

10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Waefeso 6:10

11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Waefeso 6:11

12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 6:12

13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Waefeso 6:13

14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
Waefeso 6:14

15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
Waefeso 6:15

16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Waefeso 6:16

17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Waefeso 6:17

18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Waefeso 6:18

View Details

Karibu msikilizaji katika kipindi Cha kaa tuongee ikiwa ni kwa mara ya Kwanza kabisa Leo tunaongelea swala kubwa KUJIFUNZA na KUWEKA BIDII

View Details

WAFILIPI 4:18-19

View Details

2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.
Obadia 1:2

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
Obadia 1:3

4 Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana.
Obadia 1:4

7 Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hata mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
Obadia 1:7

12 Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
Obadia 1:12

13 Usiingie katika lango la watu wangu, siku ya msiba wao; naam, usiyatazame mateso yao, siku ya msiba wao; wala usitie mikono yako juu ya mali zao, siku ya msiba wao.
Obadia 1:13

14 Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki.
Obadia 1:14

View Details

1Wakorintho 10:11-16

View Details

  1. Tambua maisha yana badilika hayapo moja kwa moja (life is not linear)

  2. Weka mipango mipya kila siku(Put new planning daily)

  3. Chunja mawanzo yako (Filter your thoughts)

View Details

"Nafasi ya kijana katika Utumishi ni kubwa sana, wewe kijana unanafasu gani katika Utumishi?. Maana vijana tuna nguvu Kuna Mithali ya kiafrika naipenda inasema "Vijana tunaweza kutembea haraka lakini wazee wanaijua njia".

View Details

Karibu kwenye ujio mpya wa nukuu za maisha ni kila siku saa nne usiku kuanzia tarehe 06/08/2020

View Details

MATHAYO 5:1-10
Karibu siku ya leo ungane nami katika maombi ya letayo Heri katikati maisha Bwana atakupogania

Mara baada ya kusikiliza podcast kama utakuwa na hitaji binafsi ka maombi andika tu kwenye Comment nahitaji maombi au wasiliana nami kwa namba nilizo kutaji kwenye podcast . Nami nitaomba kwa ajili yako

View Details

18 Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
Mithali 30:18

19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana.
Mithali 30:19

20 Hivyo ndivyo mwendo wa mwanamke mzinifu; Hula, akapangusa kinywa chake, Akasema, Sikufanya uovu.
Mithali 30:20

21 Kwa ajili ya mambo matatu nchi hutetemeka, Naam, kwa ajili ya manne haiwezi kuvumilia.
Mithali 30:21

22 Mtumwa apatapo kuwa mfalme; Mpumbavu ashibapo chakula;
Mithali 30:22

23 Mwanamke mwenye kuchukiza aolewapo; Na mjakazi aliye mrithi wa bibi yake.
Mithali 30:23

24 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.
Mithali 30:24

25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.
Mithali 30:25

26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.
Mithali 30:26

27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
Mithali 30:27

28 Mjusi hushika kwa mikono yake; Lakini yumo majumbani mwa wafalme.
Mithali 30:28

29 Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
Mithali 30:29

30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;
Mithali 30:30

31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki.
Mithali 30:31

32 Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza; Au ikiwa umewaza mabaya; Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
Mithali 30:32

View Details

Mambo matatu ya msingi unapoanza wiki mpya

  1. Usiamke na mawazo ya wiki ambayo imeisha

  2. Amka mapema sana weka mipaka yako vizuri

  3. Usiamke na kukimbilia kwenye simu bali amka mshukuru Mungu, kwa wiki ambayo imeisha na wiki unayoianza panda mbegu.

View Details

TESTIMONY THE BRIDGE OF VICTORY ushuhuda daraja la mafanikio.

Karibu kwenye program mpya ya ushuhuda daraja la ushidi hapa utapata kusikiliza shuhuda mbalimbali ambazo zitakupa kujifunza Kila siku na hamasa ya kuona upo uwezekana kwa yale ambayo unapitia

Leo nilikuwa na Baba yangu mkubwa Henry Siwiti ambaye aliugua kwa Muda mrefu sana zaidi ya miaka 32 leo Ni mzima na kumbukumbu zimerudi.